Saturday, December 17, 2016

OSCAR MBIONI KWENDA CHINA

MENEJA wa Chelsea Antonio Conte anaamini Fedha nyingi zinazotumiwa na Klabu za China kununua Wachezaji ni kitu ‘hatari kwa Timu zote Duniani’.
Hivi sasa Kiungo wa Chelsea, Oscar mwenye Miaka 25, anakaribia kujiunga na Klabu inayocheza Supa Ligi ya China, Shanghai SIPG, kwa Dau la Pauni Milioni 60 Uhamisho ambao unatarajiwa kukamilika Mwezi Januari na Mchezaji huyo kulipwa Mshahara wa Pauni 400,000 kwa Wiki.
Conte amekiri ni ngumu kumbakisha Mchezaji anayepewa Ofay a aina hiyo.
Kwa ajili ya Msimu wa 2016, Klabu za China zimetumia Pauni Milioni 200 kununua Wachezaji na ndani ya Siku 10 tu Rekodi ya Dau kubwa la kununua Mchezaji huko China lilivunjwa mara 3.

Kiungo wa Chelsea, Ramires, alisainiwa kwa Pauni Milioni 25 na Jiangsu Suning mwanzoni mwa Msimu kisha Guangzhou Evergrande Taobao ikamnunua Staa wa Colombia Jackson Martinez Kwa Pauni Milioni 31 kutoka Atletico Madrid.
Siku 3 baadae, Shanghai SIPG ikailipa Zenit St Petersburg Pauni Milioni 46.1 kumnunua Straika wa Brazil Hulk.

Dirisha la Uhamisho huko China litafunguliwa tena Januari Mosi na kufungwa Februari 28 na miongoni wanaotajwa kukumbwa na Uhamisho huo ni Fowadi wa Arsenal Alexis Sanchez ambae anadaiwa kupewa Ofay a Mshahara wa Pauni 500,000 kwa Wiki na Klabu ya Hebei China Fortune ambayo Meneja wake ni Bosi wa zamani wa Manchester City Manuel Pellegrini.

Akiongelea hali hii, Antonio Conte amekiri: “Soko la China ni hatari kwa Dunia nzima na si Chelsea tu!”

Kuhusu Oscar, Conte alikataa kuthibitisha hilo na kutaka Watu wavute subira.