Sunday, December 4, 2016

STRAIKA WA TIMU YA VIJANA MBAO FC U-20 ISMAIL MRISHO HALFAN AFARIKI DUNIA.

Ismail Mrisho Halfan alifariki akiwa njiani kuelekea Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kagera iliyoko katika Manispaa ya Bukoba.

Habari mbaya kwa Timu ya Mbao U20: Mchezaji wao Straika jezi namba 4 ISMAIL MRISHO HALFAN amefariki Dunia jioni hii baada ya kuanguka Uwanjani Kaitaba wakati wa Mtanange wao Mwadui. Amefariki Hospitali ya Goverment mjini Bukoba. Mrisho Halfan ndie aliyeifungia bao la kwanza na bao la pili lilifungwa kwa mkwaju wa Penati hivyo mtanange kumalizika kwa 2-0.
ISMAIL MRISHO HALFAN wa tatu kutoka (kushoto) muda mfupi kabla ya Mtanange wao kuanza leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba. Picha zote na Faustine Ruta.