Tuesday, December 6, 2016

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: FC BASEL 1 vs 4 ARSENAL

Arsenal wamemaliza Mechi za Kundi A la UEFA CHAMPIONS LIGI, wakiwa kileleni baada ya kuibamiza FC Basel 4-1 huko Uswisi wakati wenzao Paris Saint Germain wakitoka Sare 2-2 huko Paris.
PSG sasa wanashika Nafasi ya Pili na hivyo wao na Arsenal wanatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL wakati Ludogorets Razgrad, waliomaliza Nafasi ya 3, wanatumbukizwa Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI.
Kwenye Kundi B, Napoli iliifunga Benfica 2-1 huko Ureno na Dynamo Kiev kuichapa Besiktas 6-0 na matokeo haya yanazifanya Napoli na Benfica zifuzu Raundi ya Mtoano wakati Besiktas ikitupwa EUROPA LIGI.
Dynamo Kiev walishatupwa nje kabla ya Mechi za Jana.
Katika Kundi C, ambalo likuwa likikamilisha Ratiba tu kwa vile Barcelona walishatwaa ushindi wa Kundi, Man City kuchukua Nafasi ya Pili na Borussia Monchengladbach kutupwa Nafasi ya 3 na hivyo kupelekwa EUROPA LIGI.
Jana Barca iliichapa Borussia Monchengladbach 4-0 na City kutoka Sare na Celtic.