Tuesday, December 20, 2016

VARDY: RUFAA YATUPWA KIFUNGO KIPO PALE PALE MECHI 3!

Straika wa Mabingwa wa England Leicester City anaechezea England Jamie Vardy sasa atakosa Mechi 3 baada ya Rufaa yake kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Jumamosi Leicester ikitoka 2-2 na Stoke City kutupiliwa mbali.

Vardy, mwenye Miaka 29, atazikosa Mechi za Leicester dhidi ya Everton, West Ham na Middlesbrough.

Vardy alitolewa nje na Refa Craig Pawson katika Dakika ya 28 kwa Rafu ya Miguu Miwili kwa Straika wa Stoke Mame Diouf.