Monday, December 5, 2016

VIFUNGO: AGUERO MECHI 4, FERNANDINHO 3!

FA, Chama cha Soka England, kimemfungia Fowadi wa Manchester City Sergio Aguero Mechi 4 kwa kumchezea Rafu mbaya Beki wa Chelsea David Luis.
Tukio hilo lilitokea kwenye Mechi ya Jumamosi iliyopita ambayo City walifungwa 3-1 na Chelsea.
Aguero alicheza rafu hiyo mbaya katka Dakika za Majeruhi na kupewa Kadi Nyekundu ambayo kawaida Kifungo chake ni Mechi 3 tu.
Lakini kwa vile Aguero alishawahi kufungiwa Mechi 3 Mwezi Agosti kwa kumpiga kiwiko Mchezaji wa West Ham Winston Reid, Kifungo cha sasa kimeongezwa Mechi 1 zaidi.
Kifungo hicho cha Aguero kitamfanya azikose Mechi za City dhidi ya Leicester, Watford, Arsenal na Hull.

Manchester City news: Sergio Aguero and Fernandinho have bans confirmed following red cards v ChelseaKwenye Mechi hiyo hiyo ya City na Chelsea Kiungo wa City Fernandinho nae alitolewa kwa Kadi Nyekundu baada ya kugombana na Mchezaji wa Chelsea Cesc Fabregas katika mgongano uliofuatia rabsha za Wachezaji wa pande zote mbili mara baada ya Rafu ya Aguero.