Saturday, December 17, 2016

VPL KUANZA LEO MABINGWA YANGA NA JKT RUVU, MBEYA CITY vs KAGERA SUGAR, VINARA SIMBA JUMAPILI NANGWANDA NA NDANDA FC!

MABINGWA wa Soka Tanzania Bara, Yanga, Leo wanaanza Raundi ya Pili ya VPL, Ligi Kuu Vodacom, kwa kucheza na JKT Ruvu Uwanja wa Uhuru Jiini Dar es Salaam.
Hii Leo Yanga watakuwa na Kocha Mkuu Mpya kutoka Zambia George Lwandamina aliemrithi Hans van de Pluijm ambaeamekuwa Mkurugenzi wa Ufundi.
Pia Yanga, ambao wako Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Simba, hii Leo wataingia Uwanjani wakiwa na Wachezaji Wapya Wawili baada ya kumsaini Kiungo kutoka Zambia Justin Zulu na Straika kutoka JKU ya Zanzibar Emmanuel Martin Joseph.

Mbali ya Mechi hii ya Yanga hii Leo pia zipo mechi nyingine 3 wakati Jumapili zipo Mechi 4 za VPL ikiwemo ile ya Vinara Simba huko Nangwanda, Mtwara wakicheza na Nda Nda FC.

Nyingine Jumapili ni ile ya Timu ya 3 Azam FC ambao ni Wageni huko Uhuru Stadium Jijini Dar Es Salaam kuivaa African Lyon.

VPL
Msimamo – Timu za Juu:

1- Simba Mechi 15 Pointi 35
2- Yanga Mechi 15 Pointi 33
3- Azam Mechi 15 Pointi 25
4- Kagera Mechi 15 Pointi 24
5- Mtibwa Mechi 15 Pointi 23
VPL
Ligi Kuu Vodacom
Mechi za Mzunguko wa Pili
Ratiba
Jumamosi Desemba 17

JKT Ruvu v Yanga [Uhuru Stadium, Dar es Salaam]
Mbeya City v Kagera Sugar [Sokoine, Mbeya]
Ruvu Shhoting v Mtibwa Sugar [Mabatini, Mlandizi]
Mwadui FC v Toto African [Mwadui Complex, Mwadui]
 

Jumapili Desemba 18
Mbao FC v Stand United [CCM Kirumba, Mwanza]
Ndanda FC v Simba [Nangwanda, Mtwara]
African Lyon v Azam FC [Uhuru Stadium, Dar es Salaam]
Tanzania Prisons v Majimaji FC [Sokoine, Mbeya]