Saturday, December 17, 2016

VPL: JKT RUVU 0 vs 3 YANGA

MABINGWA wa Soka Tanzania Bara, Yanga, Leo wameanza Raundi ya Pili ya VPL, Ligi Kuu Vodacom, kwa kuibonda JKT Ruvu 3-0 huko Uwanja wa Uhuru Jiini Dar es Salaam na kushika uongozi wa Ligi hiyo.
Yanga, ambao Leo walicheza Mechi yao ya kwanza ya VPL chini ya Kocha Mkuu Mpya kutoka Zambia George Lwandamina, walifunga Bao zao 3 kupitia Michael Aidan, aliejifunga mwenyewe katika Dakika ya 38, na Bao 2 za Simon Msuva, Dakika za 57 na 93.
Ushindi huu umewaweka Yanga Nambari Wabi kwenye VPL wakiwa na Pointi 36 kwa Mechi 16 na wanafuata Simba wenye Pointi 35 kwa Mechi 15.
VPL itaendelea tena Jumapili ambapo zipo Mechi 4 za VPL ikiwemo ile ya Vinara Simba huko Nangwanda, Mtwara wakicheza na Ndanda FC.
Nyingine Jumapili ni ile ya Timu ya 3 Azam FC ambao ni Wageni huko Uhuru Stadium Jijini Dar Es Salaam kuivaa African Lyon.
Amis Tambwe akiwania mpira na beki wa JKT Ruvu.
Moja ya hatari langoni mwa JKT Ruvu.
Donald Ngoma (kushoto), akimpongeza Simon Msuva baada ya kufunga bao la pili.
Raha ya ushindi.
Simon Msuva akishangilia bao la tatu aliloifungia timu yake.