Wednesday, January 18, 2017

AZAM FC, MBEYA CITY ZAFUTANA SHATI LEO, ZATOKA SARE YA 0-0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Ligi kuu ya Vodacom imeendelea leo katika viwanja mbali mbali huku katika mchezo wa uliozikutanisha timu ya Azam Fc na Mbeya City ukimalizika kwa suluhu ya timu hizo kushindwa kufungana.

Katika mchezo huo ambao ulianza saa moja usiku katika uwanja wa Chamazi Complex uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani wa aina yake kwa timu zote zikishambuliana kwa vipindi na kucheza kwa kujiamini na kujituma kuhakikisha wanajaribu kupata ushindi lakini bahati aikuwa upande wowote.

Katika mchezo huo ambao mbeya City imeweza kucheza na wachezaji wawili ambao washawahi kuchezea timu ya Azam ambao ni Mrisho Ngassa na Zahoro Pazi na kuonyesha kuwa mwiba kwa timu hiyo kwa kujaribu kulishambulia lango la timu yao ya zamani mara kadhaa.

Mrisho Ngassa ambaye ameingia katika kipindi cha pili mara baada ya kutoka kwa Tito Okelo ameweza kufanya mabadiliko makubwa katika safu ya ushambuliaji kwa kuwa tishio katika lango la Azam Fc.
Ngasa ambaye ameweza kucheza kwa kuonyesha uzoefu wa hali ya juu kwa kuweza kusaidia upande wa kati na kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki kutokana na staili yake ya mchezo .