Thursday, January 12, 2017

COPA DEL REY: SUAREZ, NEYMAR, MESSI WAIPENYEZA BARCA ROBO FAINALI KWA KUICHAPA BAO 3-1 ATHLETICO BILBAO

Barcelona defeated Athletic Bilbao 3-1 on Wednesday.BAO za Suarez, Neymar na Messi zimewapeleka Mabingwa Watetezi FC Barcelona Robo Fainali ya Copa del Rey, Kombe la Mfalme wa Spain, walipoifunga Athletic Bilbao 3-1 huko Nou Camp hapo Jana.

Wakiwa wamefungwa 2-1 katika Mechi ya Kwanza, Barca walitangulia kufunga Dakika ya 36 kwa Bao la Luis Suarez likiwa Bao lake la 100 katika Mechi 120 za Barca.

Neymar aliongeza Bao la Pili Dakika ya 47 na Bilbao kupiga Bao lao moja Dakika ya 51 kupitia Saborit na kufanya Gemu iwe Sare 3-3 kwa Mechi 2 lakini Messi akapiga Bao la 3 Dakika ya 70 na kuwapa Barca ushindi wa 3-1 na 4-3 kwa Mechi Mbili.