Wednesday, January 11, 2017

DIAMOND AKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA KUTUMBUIZA UZINDUZI WA AFCON

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (Kushoto) akikabidhi Bendera ya Taifa kwa Mwanamuziki wa nyimbo za Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ Dar es Salaam leo, kabla ya kwenda kuliwakilisha Taifa kwa kufanya shoo wakati wa ufunguzi wa michuano ya Soka Barani Afrika (AFCON 2017). Wapili kulia ni Balozi wa DStv, Lucas Mhavile ‘Joti’.