Friday, January 27, 2017

EFL CUP: MAN UNITED WAPOTEZA LAKINI WATINGA FAINALI SASA NI WAO DHIDI YA SOUTHAMPTON

Hull City waliifunga Manchester United 2-1 katika Mechi ya Pili ya Nusu Fainali yaEFL CUP, ambalo ndio Kombe la Ligi huko England, iliyochezwa huko KCOM Stadium lakini Fainali ni Man United dhidi ya Southampton.
Kipigo hicho kimemaliza wimbi la kutofungwa Mechi 17 lakini Man United wamesonga Fainali kwa Jumla ya Mabao 3-2 baada ya kushinda Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali huko Old Trafford Bao 2-0.

Wakichezesha Kikosi kilichobadilishwa Wachezaji Watano kilijikuta kiko nyuma kwa Bao 1-0 katika Dakika ya 35 kwa Penati ya Dakika ya 35 iliyopigwa na Tom Huddlestone Penati ambayo ilikuwa tata.
Man United walisawazisha Dakika ya 66 kupitia Paul Pogba na Hull City kufunga Bao lao la pili na la ushindi katika Dakika ya 85 Mfungaji akiwa Oumar Nasse.

Fainali ya EFL CUP itachezwa huko London Uwanjani Wembley hapo Februari 26 na Man United kuwa na nafasi ya kutwaa Taji la Pili Msimu huu baada ya kubeba Ngao ya Jamii mwanzoni mwa Msimu ikiwa watawafunga Southampton.
Southampton, maarufu kama ‘Watakatifu’, Juzi waliwabwaga Liverpool 1-0 na kusonga Fainali kwa Jumla ya Mabao 2-0.


VIKOSI:
HULL CITY:
Marshall, Meyler, Maguire, Dawson, Tymon, Huddlestone, Clucas, Niasse, Maloney, Diomande, Bowen
Akiba: Robertson, Hernández, Kuciak, Elabdellaoui, Weir, Goebel, Markovic
MANCHESTER UNITED: De Gea, Darmian, Jones, Smalling, Rojo, Carrick, Herrera, Lingard, Pogba, Rashford, Ibrahimovic.
Akiba: Romero, Fosu-Mensah, Shaw, Fellaini, Mata, Mkhitaryan, Rooney
REFA: Jonathan Moss