Thursday, January 12, 2017

EFL CUP – NUSU FAINALI: SOUTHAMPTON 1 v 0 LIVERPOOL

Southampton imeifunga Liverpool 1-0 huko Saint Mary hapo Jana katika Mechi yao ya Kwanza ya Nusu Fainali ya EFL CUP, ambalo ndio Kombe la Ligi huko England.
Juzi, kwenye Mechi nyingine ya Kwanza ya Nusu Fainali nyingine iliyochezwa Old Trafford, Manchester United iliichapa Hull City Bao 2-0 kwa Bao za Juan Mata na Marouane Fellaini.
Bao la ushindi la Southampton, ambao ni maarufu kama ‘Watakatifu’, hapo Jana lilifungwa na Nathan Redmond baada kupokea Pasi ya Jay Rodriguez katika Dakika ya 20. Van Dijk blocks a shot from Roberto FirminoSouthampton wamgeweza kupata Bao nyingi kama si ushujaa wa Kipa wa Liverpool Loris Karius alieokoa Mipira mingi na hasa mara 2 kufuta kwenye chaki ya Goli Mipira ya Nathan Redmond.
Daniel Sturridge battles for the ball with Vigril van DijkNusu Fainali hizi huchezwa kwa Mikondo Miwili ya Nyumbani na Ugenini na hivyo Marudiano ya Mechi hizi yatakuwa hapo Januari 25 na 26 huko Anfield na KCOM Stadium. Lucas and Jay Rodriguez battle for the ball in the first halfEFL CUP
Nusu Fainali
MARUDIANO
Jumatano Januari 25

23:00 Liverpool v Southampton [0-1]
Alhamisi Januari 26
22:45 Hull City v Manchester United [0-2]