Tuesday, January 31, 2017

EMIRATES FA CUP: DROO RAUNDI YA 5: BLACKBURN ROVERS vs MAN UNITED SUTTON UNITED vs ARSENAL

DROO ya Raundi ya 5 ya EMIRATES FA CUP, Kombe Kongwe Duniani, imefanyika Jana na hakuna Mechi yeyote itakayokutanisha Timu za EPL, Ligi Kuu England, pekee wakati Mabingwa Watetezi Manchester United walipopangwa Ugenini huko Ewood Park kucheza na Blackburn Rovers ambayo sasa ipo Daraja la chini.

Sutton United, moja ya Timu mbili ambazo haipo kwenye Mfumo rasmi wa Ligi na imetinga Raundi hii, wapo Nyumbani kuwakaribisha Arsenal ambao wametwaa FA CUP mara 12 wakiongoza pamoja na Man United kwa wingi wa kulibeba.

Timu ya Pili isiyo kwenye Ligi, Lincoln City, wao wapo Ugenini kucheza na Timu ya EPL, Burnley.
Vinara wa EPL Chelsea wapo Ugenini kucheza na Wababe wa Liverpool, Wolves wakati Manchester City wapo Ugenini kwa Huddersfield ambao wako Daraja la Championship ambamo pia wako Fulham watakaokuwa Wenyeji wa Tottenham.

Mechi 8 za Raundi ya 5 zitachezwa kati ya Ijumaa Februari 17 na Jumatatu Februari 20.
DROO KAMILI:

Burnley v Lincoln City
Fulham v Tottenham Hotspur
Blackburn Rovers v Manchester United
Sutton United v Arsenal
Middlesbrough v Oxford United
Wolverhampton Wanderers v Chelsea
Huddersfield Town v Manchester City
Millwall v Derby County/Leicester City