Thursday, January 5, 2017

EPL: TOTTENHAM HOTSPUR 2 vs 0 CHELSEA, DELE ALLI AONESHA KIWANGO KIKUBWA KWA DABI YAO, CHELSEA WACHAPWA!


Dabi ya Jiji la London ilipigwa Uwanjani White Hart Lane na Tottenham Hotspur kuibuka kidedea kwa ushujaa wa Dele Alli kuwabwagaVinara wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea Bao 2-0 na kuifyeka ndoto yao ya kuweka Rekodi ya ushindi wa Mechi 14 mfululizo kwenye Ligi hiyo.
Huku Timu zote zikitumia Mfumo wa aina moja, 3-4-3, Gemu ilichezwa sana kati kulikokuwa na lundo la la Wachezaji lakini Kipindi cha Kwanza chote Spurs walionekana wako ngangari na kutawala na kuleta kosakosa kadhaa langoni mwa Chelsea.

Presha yao ilitoa majibu pale Walker alipochomoka na Mpira na kumzidi maarifa Alonso na kisha kumrudishia Mpira Eriksen alietoa Krosi iliyounganishwa na Dele Alli kwa Kichwa ikimwacha Kipa Courtois akilala hoi na kutinga wavuni kuwaandikia Bao Dakika ya 46.
Hadi Haftaimu, Spurs 1 Chelsea 0.
Dakika ya 53, Spurs wakaenda 2-0 mbele baada ya Krosi ya Eriksen kuunganishwa kwa Kichwa na Dele Alli hadi wavuni.
Hii ilikuwa ni Mechi ya mwisho ya EPL baada kuchezwa Mechi mfululizo toka Krismasi na sasa inaenda Vakesheni kupisha Mechi za Raundi ya 3 ya FA CUP zinazoanza Ijumaa Usiku.
EPL itarejea dimbani Jumamosi Januari 14.


JE WAJUA?
-Tottenham wameshinda Mechi 5 tu kati ya Mechi 49 za Ligi dhidi ya Chelsea wakitoka Sare 19 na Kufungwa 26 lakini Mechi zao zote 5 za ushindi zilikuwa Uwanjani White Hart Lane.
-Katika Mechi 10 zilizopita za EPL Uwanjani White Hart Lane, Chelsea wameshinda mara 1 tu, 4-2 hapo Oktoba 2012 nyingine ni Sare 5 Kufungwa 5.