Wednesday, January 11, 2017

FIFA YAPITISHA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA KUWA NA TIMU 48


FAINALI za Kombe la Dunia zitapanuliwa na kushirikisha Nchi 48 kutoka 32 za hivi sasa.
Mabadiliko hayo yamepitishwa Leo huko Zurich, Uswisi kwa Kura nyingi na yataanza kwenye Fainali za Mwaka 2026 ambazo bado hazijapata Mwenyeji.
Fainali zijazo zitachezwa huko Russia Mwaka 2018 na zinazofuata ni huko Qatar Mwaka 2022 na zote zitakuwa na Timu 32 tu.
Kwenye Mfumo wa Timu 48 kwenye Fainali, Mechi za Awali zitakuwa za Makundi 16 ya Timu 3 kila moja ambayo yatatoa Timu 32 kwenda Raundi ya Mtoano.

Kwa Mfumo huo mpya Jumla ya Mechi kwenye Fainali zitakuwa 80 kutoka 64 za sasa lakini Bingwa wa Dunia atacheza Mechi 7 tu kama ilivyo sasa ambazo zote zitakamilika ndani ya Siku 32.
Hii ni mara ya kwanza kwa FIFA kuongeza idadi ya Timu kwenye Fainali za Kombe la Dunia tangu zilipopanuliwa Mwaka 1998 na kuwa za Timu 32 kutoka 24.
Kwa mujibu wa tafiti za FIFA upanuzi huu utafanya Mapato yaongezeke na kuwa Pauni Bilioni 5.29 na kuleta Faida kuwa Pauni Milioni 521.

FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA - Timu 48:
-Makundi: Mechi 2

-Raundi ya Mtoano ya Timu 32
-Raundi ya Mtoano ya Timu 16
-Robo Fainali
-Nusu Fainali
-Fainali