Sunday, January 22, 2017

FULL TIME...ARSENAL 2 vs 1 BURNLEY

Arsenal wakiwa kwao Emirates wamefanikiwa kushinda 2-1 kwa Penati Dakika za Majeruhi wakati wakiwa Mtu 10 na pia kumpoteza Meneja wao Arsene Wenger alietolewa nje ya Uwanja na Refa.
Ushindi huo umewaweka Arsenal Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 6 nyuma ya Vinara Chelsea ambao wanacheza baadae Leo na wakiwa Pointi 1 mbele ya Timu ya 3 Tottenham.
Arsenal walitangulia kufunga Dakika ya 59 kwa Bao la Sentahafu wao Mustafi lakini Dakika ya 65 wakabaki Mtu 10 baada Kiungo wao Xhaka kupewa Kadi Nyekundu.

Burnley walisawazisha kwa Penati ya Dakika za Majeruhi zilizoongezwa 7 kupitia Gray katika Dakika ya 93 baada ya Refa Jon Moss kuamua Francis Coquelin alimchezea Faulo Ashley Barnes na Andre Gray kusawazisha.

Tukio hilo lilimfanya Wenger alalamike sana na Refa Moss kumtimua Uwanjani.

Lakini Refa huyo, katika Dakika ya 98, aliwapa Arsenal Penati baada kuamua Buti ya Ben Mee ilikuwa juu Kichani mwaLaurent Koscielny na Alexis Sanchez kufunga Bao la Pili na la ushindi kwa Arsenal.
Mapema Leo, Southampton wakiwa kwao Saint Mary, waliwatandika Mabingwa Watetezi Leicester City 3-0 kwa Bao za Ward-Prowse, Rodriguez na Penati ya Tadic na kuwaacha Mabingwa hao wakiwa wameenda Gemu 11 za Ugenini kwenye EPL Msimu huu bila ushindi.
Sasa Leicester wapo Nafasi 3 juu ya zile Timu 3 za mkiani huku Southampton wakipanda hadi Nafasi ya 11.