Thursday, January 5, 2017

HULL CITY YAMTIMUA MENEJA MIKE PHELAN

KLABU ya Hull City imethibitisha kuachana na Meneja wao Mike Phelan alieshinda Mechi 3 tu kati ya 20.
Phelan, mwenye Miaka 54 na ambae alikuwa Msaidizi wa Sir Alex Ferguson huko Man United, aliteuliwa Meneja wa kudumu Mwezi Oktoba.
Juzi Jumatatu, Hull City ilichapwa 3-1 na West Bromwich Albion na kuiacha ikiwa eneo la hatari la mkiani mwa EPL, Ligi Kuu Engl, wakiwa na Pointi 13 kwa Mechi 20.
Phelan aliteuliwa Meneja wa Muda wa Hull mwanzoni mwa Msimu kuchukua Nafasi ya Steve Bruce ambae aliamua kuachana na Klabu hiyo ikiwa ni Miezi Miwili tu tangu aipandishe Daraja.
Msimu huu, Hull walianza vyema EPL kwa kushinda Mechi zao 2 za kwanza dhidi ya Mabingwa Watetezi Leicester na Swansea lakini baada ya hapo wakadorora na hatimae Vichapo vya hapa na pale.