Monday, January 30, 2017

JOSE MOURINHO: BASTIAN SCHWEINSTEIGER KUBAKI OLD TRAFFORD

Image result for Bastian SchweinsteigerBastian Schweinsteiger, atabakia Manchester United na kucheza kwenye UEFA EUROPA LIGI.
Uamuzi huo umetobolewa na Meneja wa Man United Jose Mourinho Jana mara baada ya kuwafunga Wigan 4-0 na kutinga Raundi ya 5 ya EMIRATES FA CUP kwenye Mechi ambayo Schweinsteiger alifunga Bao la kusisimua mno.
Mwanzoni mwa Msimu, Schweinsteiger, mwenye Miaka 32, hakujumuishwa kwenye Kikosi cha Man United kilichosajiliwa UEFA EUROPA LIGI na kuondolewa toka kwenye Kikosi cha Kwanza.
Akiongea hapo Jana, Mourinho alieleza: "Hatuna Wachezaji wengi wa Kiungo na hivyo yeye anaweza kutumika. Ataingizwa Listi ya EUROPA LIGI kwa sababu zipo nafasi baada kuondoka Memphis Depay na Morgan Schneiderlin."
Schneiderlin aliuzwa kwa Everton Januari 12 na Siku 8 baadae Depay akahamia Lyon ya France.
Mechi na Wigan ni ya 3 kwa Schweinsteiger kucheza chini ya Mourinho baada kurudishwa Kikosi cha Kwanza Mwezi Oktoba.
Man United watacheza Old Trafford na Saint-Etienne ya France kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI hapo Februari 16 na kurudiana Ugenini Wiki moja baadae.