Monday, January 30, 2017

KAGERA SUGAR YAMUENZI DAVID BURHAN KWA USHINDI DHIDI YA MTIBWA SUGAR.

Kuzikwa nyumbani kwao Mivinjeni - Iringa
Kikosi cha timu ya Mtibwa leo kilichoanza Dhidi ya Kagera Sugar. Picha na Faustine Ruta
Bao za Kagera Sugar leo zimefungwa na Mbaraka Yusuph dakika ya 29 kipindi cha kwanza na bao la pili lilifungwa na Ibrahim Twaha dakika ya 53 huku Mtibwa Sugar wakipatiwa bao lao la kufutia machozi na mchezaji wake Stamil Mbonde dakika ya 79.
Wachezaji wa Kagera Sugar wakishangilia bao la kwanza kwa aina yake lililofungwa kwa mpira wa adhabu (frii-kiki) na Mbaraka Yusuph.


TAARIFA ZA KIFO CHA DAVID BURHAN KIPA WA KAGERA SUGAR
Kipa wa Kagera Sugar na Kipa wa zamani wa Prisons, Mbeya City, Maji Maji David Burhan amefariki katika Hospitali ya Bugando Jijini MWANZA alikokuwa Akitibiwa.

Akiongea na kituo kimoja cha radio kocha wa Mtibwa Sugar Meck Mecksime amesema David alianza kuumwa wakati wakiwa safarini kuelekea kucheza na Singida United kombe la FA, akilalamika kuumwa Tumbo , Alipopimwa baadae alikutwa na malaria hali iliyofanya viongozi wa Kagera Sugar kuamua kumwacha Biharamulo wakati wanatoka Singida kwamatibabu zaidi.

Baadae alienda hospitali ya kiwanda cha Kagera kwa matibabu zaidi lakini madaktari walipendekeza akatibiwe zaidi Bugando Mwanza ambako ndipo mauti yamemkutia.

bukobasports.com  tunawapa Pole Wazazi, Ndugu na Jamaa Uongozi, wachezaji na wapenzi wote wa Kagera Sugar, na watu wote walioguswa na Msiba huu.