Tuesday, January 31, 2017

LEO MTANANGE ANFIELD - LIVERPOOL v CHELSEA NANI KUIBUKA KIDEDEA? KLOPP ALIA NA WACHEZAJI WAKE KUFANYA KWELI!


EPL – Ligi Kuu England
RATIBA:
Saa 4 Dakika 45 Usiku 

 Jumanne Januari 31
Arsenal v Watford
Bournemouth v Crystal Palace
Burnley v Leicester City
Middlesbrough v West Bromwich Albion
Sunderland v Tottenham Hotspur
Swansea City v Southampton
2300 Liverpool v Chelsea
Daniel Sturridge & Jurgen KloppMENEJA wa Liverpool Jürgen Klopp amesisitiza Msimu wao haujapotea na Timu yake inaweza kufufua matumaini ya Ubingwa kwa Leo kuwafunga Chelsea Uwanjani Anfield kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Liverpool wameporomoka hadi Nafasi ya 4 kwenye EPL wakiwa Pointi 10 nyuma ya Vinara Chelsea walio chini ya Meneja Antonio Conte.
Ndani ya Wiki moja iliyopita, Liverpool wametupwa nje ya Makombe Mawili, EFL CUP na FA CUP, wakipokea vipigo vitatu mfululizo Nyumbani kwao Anfield ambako hawajafungwa Mechi 4 mfululizo tangu Mwaka 1923.
Kipigo cha 4 hakitaki Klopp na safari hii anacheza na Chelsea ambayo Mwezi Septemba aliichapa huko Stamford Bridge Bao 2-1.
Baada kurejea kwa Sadio Mane kikosini akitokea huko Gabon kwenye AFCON 2017 alikokuwa akiichezea Nchi yake Senegal, Klopp anaweza kuwachezesha kwa pamoja kwa mara ya kwanza tangu Novemba 6 walipoinyuka Watford 6-1, Mastaa wake kina Sadio Mané, Philippe Coutinho, Roberto Firmino na Adam Lallana ambao ni kombinesheni kali ya Mashambulizi. 


REFA: Mark Clattenburg
EPL – Ligi Kuu England
Ratiba Saa 4 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Jumatano Februari 1

West Ham United v Manchester City
2300 Manchester United v Hull City
2300 Stoke City v Everton

Jumamosi Februari 4
1530 Chelsea v Arsenal
1800 Crystal Palace v Sunderland
1800 Everton v Bournemouth
1800 Hull City v Liverpool
1800 Southampton v West Ham United
1800 Watford v Burnley
1800 West Bromwich Albion v Stoke City
2030 Tottenham Hotspur v Middlesbrough 


Jumapili Februari 5
1630 Manchester City v Swansea City
1900 Leicester City v Manchester United