Saturday, January 28, 2017

AFCON 2017: SENEGAL 0 vs 0 CAMEROON(PENATI 5-4) CAMEROON IPO NUSU FAINALI!

Fowadi wa Liverpool Sadio Mane akiwa amekaa chini akiwa hoi baada ya kukosa mkwaju wa penati.
Mchezaji wa Liverpool, Sadio Mane, amekosa penati muhimu wakati Cameroon ikiifunga Segegal magoli 5-4 kupitia mikwaju ya penati na kutinga nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Mane, ambaye ni mchezaji ghali wa Afrika kuliko wachezaji wengine penati yake ilizuiliwa na kipa Fabrice Ondoa, huku mchezaji wa Cameroon Vincent Aboubakar akifunga goli la penati la ushindi.
Senegal iliyocheza vizuri katika mchezo huo ilikuwa na nafasi kubwa ya kushinda katika muda wa kawaida, ambapo shuti la Moussa Sow lilipaa juu na kuufanya mchezo huo uliopigwa kwa dakika 120 kuishia bila goli.
Matokeo hayo yanatoa nafuu kwa Liverpool ambayo imekuwa ikimkosa Mane, huku jana ikipata kipigo cha kushtua cha magoli 2-1 kutoka timu ya Wolverhampton Wanderers katika kombe la FA.

Timu ya kina Mane wakiwa hoi baada ya kuyamaliza mashindano kwa kuondolewa kwa mikwaju ya penati

Cameroon wakipeta baada ya kushuhudia mpira wa Vincent Aboubakar wa mkwaju wa penati ukizama nyavuni
Senegal nje!

Mane akigombea mpira dhidi ya Ambroise Oyongo

Cameroon wakipeta kwa kusonga mbele

MECHI 2 za Robo Fainali za AFCON 2017, Mashindano ya 31 ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, zimechezwa Jana huko nchini Gabon na Burkina Faso na Cameroon kufuzu kuingia Nusu Fainali.
Leo zipo Mechi 2 za mwisho za Robo Fainali kati ya Congo DR na Ghana kisha Egypt na Morocco.
SENEGAL 0 vs 0 CAMEROON  [Cameroon asonga Penati 5-4]
Cameroon wameitoa Senegal kwa Mikwaju ya Penati 5-4 na kutinga Nusu Fainali ya AFCON 2017 katika Mechi iliyochezwa Stade de Franceville Mjini Franceville Nchini Gabon.

Timu hizo zilitoka 0-0 katika Dakika 120 za Mchezo na kuja Mikwaju ya Penati Tano Tano na Kipa wa Cameroon Ondoa kuwa Shujaa kwa kuokoa Penati ya mwisho ya Senegal iliyopigwa na Sadio Mane anaechezea huko England kwenye Klabu ya Liverpool.

VIKOSI:
Senegal:
Diallo, Mbodji, Koulibaly, Mbengue (Ciss 85'), Gassama, Gueye, Kouyate (Ndiaye 110'), Saivet, Diouf (Sow 65'), Mane, Balde.
Cameroon:
Ondoa, Fai, Teikeu, Ngadeu, Oyongo, Siani, Djoum (Mandjeck 102'), Moukandjo, Toko Ekambi ((Zoua 47'), Tambe (Aboubakar 102'), Bassogog.

BURKINA FASO 2 vs 0 TUNISIA

Bao 2 za Kipindi cha Pili za Aristide Bance, Dakika ya 81, na Prejuce Nakoulma, 85’, kwenye Mechi ya Robo Fainali ya AFCON 2017 huko Stade d'Angondj√© iMjini Libreville Nchini Gano Jana Usiku zimewapeleka Burkina Faso Nusu Fainali walipoilaza Tunisia.

Burkina Faso sasa watacheza na Egypt au Morocco kwenye Nusu Fainali.

VIKOSI:
Burkina Faso:
Koffi, Yago, Kone, Nakoulma, A .Traore, Dayo, Kabore, B. Traore (A. Traore 90'), Coulibaly, Bayala (Bance 75'), I. Toure (Sare 86')
Tunisia: Mathlouthi, Abdennour, Ben Youssef, Msakni, Khazri (Lahmar 63'), Khenissi (Khalifa 85'), Sassi, Ben Amor, Yacoubi, Naguez, Sliti

AFCON 2017
Ratiba:
Robo Fainali
Jumamosi Januari 28

Burkina Faso 2 Tunisia 0 [RF 1]
Senegal 0 Cameroon 0 [Penati 4-5] [RF 2]

Jumapili Januari 29
1900 Congo DR v Ghana [RF 3]
2200 Egypt v Morocco [RF 4]

Nusu Fainali
Jumatano Februari 1

22:00 Burkina Faso v Mshindi RF 4

Alhamisi Februari 2
22:00 Cameroon v Mshindi RF 3

Mshindi wa 3
Jumamosi Februari 4

2200 Aliefungwa NF 1 v Aliefungwa NF 2
Fainali
Jumapili Februari 5

2200 Mshindi NF 1 v Mshindi NF 2

NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA:
-Egypt-Mara 7
-Cameroon, Ghana-Mara 4
-Nigeria-Mara 3
-Congo DR-Mara 2
-Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan, Tunisia-Mara 1