Saturday, January 21, 2017

FULL TIME: STOKE CITY 1 vs 1 MANCHESTER UNITED, ROONEY AIBEBA UNITED NA KUWEKA REKODI UGENINI KWA KUSAWAZISHA BAO.

Wayne Rooney amekuwa Mfungaji Bora katika Historia ya Manchester United baada ya Frikiki yake ya Dakika za Majeruhi kuwapa Sare ya 1-1 walipocheza na Stoke City katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England huko Bet 365 Stadium.

Stole walitangulia kufunga katika Dakika ya 19 kwa Bao la kujifunga mwenyewe Juan Mata alietumbukiza Mpira wavuni kutokana na Krosi ya Erik Pieters.

Rooney, alieingizwa kutoka Benchi katika Dakika ya 67 kumbadili Mata, alipiga Friki ya Dakika ya 94 na kufunga Bao lake la 250 kwa Man United alimzidi aliekuwa akishikilia Rekodi Sir Bobby Charlton ya Bao 249.

Bao hilo limedumisha Rekodi ya Man United ya kutofungwa katika Mechi 17 lakini limewaweka wakiwa Pointi 3 kutoka Timu ya 4 Arsenal na wapo Pointi 11 kutoka kwa Vinara Chelsea.
Juan Mata kawapa zawadi Stoke City dakika ya 19 ya kipindi cha kwanza.Mata kajifunga bao dakika ya 19 na kuwapa zawadi Stoke City kipindi cha kwanza. mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika United 0 Stoke City 1.Man United kwenye harakati za kupunguza pengo na kusonga mbele...