Saturday, January 14, 2017

FULL TIME VPL: KAGERA SUGAR YAISAMBARATISHA NDANDA FC BAO 2-0 MBELE YA JAMAL MALINZI LEO KAITABA STADIUM

Saloum Umande Chama akiwa sambamba na Rais wa shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Ndugu Jamal Malinzi(kulia) ni Afisa Utamaduni Manispaa Bukoba Bw. Rugeiyamu wakiwa jukwaa kuu (meza kuu) wakiutazama mtanange huo leo jumamosi. Kagera waibuka kidedea bao 2-0.
Kikosi cha Kagera Sugar kilichoanza dhidi ya Timu ya Ndanda Fc leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Bao la kwanza la Kagera Sugar lilifungwa kipindi cha kwanza dakika ya 24 kupitia kwa mfungaji wake matata Mbaraka Yusuph na kwenda mapumziko kwa bao 1-0. Kipindi cha pili Kagera Sugar walipata penati na kuumaliza mtanange huo kwa bao 2-0 huku Ndanda Fc wakiumaliza pungufu 10 uwanjani kwa mchezaji wake Salvatory  kupata kadi ya pili ya njano na kisha kuoneshwa kadi nyekundu.
Mchezo huo pia umeshuhudiwa na Rais wa TFF Jamal Malinzi kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mtu Kati!

1-0

Ligi Kuu Vodacom, imeendelea Leo kwenye Viwanja Viwili na kushuhudia Timu za Nyumbani zote zikishinda 2-0.
Huko Shinyanga, Stand United imewacharaza wenzao wa Mkoa huo Mwadui FC Bao 2-0 kwa Bao za Jacob Massawe na Adeyum Salehe na kujikita Nafasi ya 6 wakati Mwadui wapo wa 10.


Kiongozi wa Ndanda Fc akitoa onyo
Ushindi huu umewaweka Kagera Sugar Nafasi ya 3 wakiwa na alama 31 wakati Ndanda FC wakiwa nafasi ya 13.
VPL itaendelea Jumapili kwa Mechi 1 huko CCM Kirumba, Mwanza kati ya Mbao FC na African Lyon.