Thursday, January 19, 2017

MANCHESTER UNITED NDIO KLABU YENYE MAPATO MAKUBWA DUNIANI, BARCELONA NAO JUU..REAL INAFUATIA.


Manchester United ndio Klabu iliyovuna Mapato makubwa kupita yeyote Duniani kwa Msimu uliopita kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na Deloitte, Magwiji wa Mahesabu na Fedha Duniani.
Man United imewabwaga waliokuwa wakiongoza Listi ya Klabu Tajiri Kimapato, Real Madrid, ambao walikaa huko kileleni kwa Miaka 11.
Wakichukua Nambari Wani, Man United wamevuna Mapato ya Pauni Milioni 515 kwa Msimu wa 2015/16.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa Man United kuchukua uongozi wa Listi ya Deloitte tangu Msimu wa 2003/04.

Nafasi ya Pili imeshikwa na Barcelona na Real Madrid ni wa 3 huku Bayern Munich wakiwa wa 4 na Man City ni wa 5.
Katika 20 Bora ya Listi hiyo zipo Klabu 8 za EPL, Ligi Kuu England huku Mabingwa wa England Leicester City wakitinga humo kwa mara ya kwanza.Arsenal, Chelsea, Liverpool na Tottenham zimebakia Nafasi za 7, 8, 9 na 12 huku West Ham wakishika Nafasi ta 18.

LISTI YA DELOITTE - 10 BORA:

*Timu, (Kwenye Mabano Nafasi Msimu uliopita), Mapato Msimu 2015/16 (Mapato 2014/15)
1 (3) Manchester United689 (515.3)519.5 (395.2)
2 (2) Barcelona620.2 (463.8)560.8 (426.6)
3 (1) Real Madrid620.1 (463.8)577 (439)
4 (5) Bayern Munich592 (442.7)474 (360.6)
5 (6) Manchester City524.9 (392.6)463.5 (352.6)
6 (4) Paris St-Germain520.9 (389.6)480.8 (365.8)
7 (7) Arsenal468.5 (350.4)435.5 (331.3)
8 (8) Chelsea447.4 (334.6)420 (319.5)
9 (9) Liverpool403.8 (302)391.8 (298.1)
10 (10) Juventus341.1 (255.1)323.9 (246.4)