Saturday, January 14, 2017

MAPINDUZI CUP: HIMID MAO AIPA AZAM FC KOMBE, KWA BAO 1-0 DHIDI YA SIMBA

HIMID MAO amepeleka Kombe la Mapinduzi ambayo ni Mashindano ya kuenzi Miaka 53 ya Mapinduzi Tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba, kwa Bao lake pekee wakati Azam FC ikifunga Simba 1-0 Uwanjani Amaan Stadium huko Zanzibar Jana Usiku.
Mao alifunga Bao hilo Dakika ya 13 kwa Shuti kali la Mita 25 ambalo Kipa wa Simba Daniel Agyei hakuona ndani.
Baada ya Mechi hiyo Nahodha wa Azam FC, John Bocco, alikabidhiwa Kombe la Mapinduzi na Rais wa Zanzibar, Dokta Ali Mohammed Shein.

Simba waltinga Fainali hii kwa mbwembwe kubwa baada ya kuwabwaga Watani zao Yanga kwa Mikwaju ya Penati 4-2 na Washabiki wao wengi waliamini hilo liliwafanya wastahili Kombe la kini Azam FC, wakiwa chini ya Kocha wa muda, Idd Cheche, walikuwa na stori nyingine kabisa.

Sasa Timu hizi zote zinarejea Bara kucheza VPL, Ligi Kuu Vidacom, ambapo Simba watakuwa dimbani Jumatano huko Jamhuri, Morogoro kuivaa Mtibwa Sugar na Siku hiyo hiyo Azam FC kuwa kwao Chamazi kucheza na Mbeya City.

VIKOSI VILIVYOANZA:

AZAM FC:
Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gardiel Michael, Aggrey Moris, Yakubu Mohammed, Stephan Mpondo, Joseph Mahundi, Salum Abubakar, John Bocco, Yahya Mohammed, Himid Mao.

SIMBA:
Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein, Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, James Kotei, Juma Luizio, Muzamiru Yassin, Mwinyi Kazimoto