Wednesday, January 18, 2017

MEMPHIS DEPAY KUTIMKIA UFARANSA KWENYE KLABU YA LYON

Memphis Depay.
Manchester United wameafiki dili ya kumuuza Memphis Depay kwa Klabu ya France Lyon.
Inaaminika Ada ya Uhamisho ni Pauni Milioni 16 na kupanda hadi Pauni Milioni 21.7 ikitegemea vigezo kadhaa vikiwemo Lyon kufuzu kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI na Depay kuongezewa Mkataba.
Pia kwenye Mkataba wa Mauzo wa Mchezaji huyo vipo Vipengeli vinvyohusu Man United kumnunua tena na pia kuhusishwa akiuzwa kwa Klabu nyingine.
Depay, mwenye Miaka 22 na ambae huichezea Timu ya Taifa ya Netherlands, amefunga Bao 7 kwa Man United katika Mechi zake 53 alizocheza tangu ajiunge kutoka PSV Eindhoven Mei 2015 kwa Dau la Pauni Milioni 25.

Msimu huu, Depay ameichezea Man United Mechi 8 tu lakini tangu Oktoba amecheza Dakika 8 tu.
Katika kipindi hiki cha Dirisha la Uhamisho la Januari, Depay amekuwa Mchezaji wa Pili kuuzwa na Man United na mwingine ni Morgan Schneiderlin alieuzwa kwa Everton Januari 12 kwa Ada ya Pauni Milioni 24.