Monday, January 30, 2017

RATIBA/LIGI KUU ENGLAND HIYO TENA, YAREJEA, JUMANNE ANFIELD NI LIVERPOOL vs CHELSEA, JUMATANO MAN UNITED vs HULL CITY OLD TRAFFORD

Baada kupisha Mechi za EFL CUP na FA CUP, EPL, Ligi Kuu England, inarejea kwa kishindo Jumanne Usiku kwa Mechi 7 na Jumatano Mechi 3 huku Macho yapo Anfield ambako Liverpool ‘goigoi’ ataukwaa moto wa Vinara wa Ligi hiyo Chelsea.

Hivi sasa Liverpool wapo mrama baada ya kushinda Mechi 1 tu kati ya 8 za Mashindano yote waliyocheza Mwaka huu 2017.

Ndani ya Siku 4 Wiki iliyopita, Liverpool walitupwa nje ya Makombe Mawili, EFL CUP na FA CUP, na kilichouma zaidi Mechi zote wamepigiwa kwao Anfield na uchungu zaidi ni Wikiendi kutupwa nje ya FA CUP na Timu ya Daraja la chini Wolverhampton Wanderers.
Kwenye EPL, Liverpool wapo Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 10 nyuma ya Vinara Chelsea.
Mechi nyingine za Jumanne Usiku ni huko Emirates kati ya Arsenal na Watford wakati Mabingwa Watetezi Leicester City, ambao wanasuasua, wapo Ugenini kucheza na Burnley na huko Stadium of Light, Timu ya Mkiani, Sunderland itawakaribisha Tottenham Hotspur ambao wako Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 9 nyuma ya Vinara Chelsea. Jumatano zipo Mechi 3 wakati huko London Stadium ni kati ya West Ham na Man City, Stoke City wakiwa Nyumbani kuivaa Everton na Man United wapo kwao Old Trafford kuivaa Hull City ambayo ndio Wiki iliyopita waliitoa kwenye Nusu Fainali ya EFL CUP licha ya Hull kuifunga Man United 2-1 huko KCOM Stadium kwani walipoteza Mechi ya kwanza Old Trafford 2-0 na hivyo kubwagwa kwa Jumla ya 3-2 kwa Mechi 2.
 

Ligi Kuu England - EPL
RATIBA:
Saa 4 Dakika 45 Usiku
Jumanne Januari 31

Arsenal v Watford
Bournemouth v Crystal Palace
Burnley v Leicester City
Middlesbrough v West Bromwich Albion
Sunderland v Tottenham Hotspur
Swansea City v Southampton
2300 Liverpool v Chelsea

Jumatano Februari 1
West Ham United v Manchester City
23:00 Manchester United v Hull City
23:00 Stoke City v Everton

Jumamosi Februari 4
1530 Chelsea v Arsenal
1800 Crystal Palace v Sunderland
1800 Everton v Bournemouth
1800 Hull City v Liverpool
1800 Southampton v West Ham United
1800 Watford v Burnley
1800 West Bromwich Albion v Stoke City
2030 Tottenham Hotspur v Middlesbrough

Jumapili Februari 5
1630 Manchester City v Swansea City 

1900 Leicester City v Manchester United