Wednesday, January 18, 2017

SIMBA NA MTIBWA WAUMALIZA KWA SARE! 0-0 KWENYE UWANJA WA JAMHURI MOROGORO LEO

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii Morogoro
Timu ya Simba imeshindwa kuondoka na ushindi kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro baada ya kulazimishwa sare ya kutokufungana na wakata miwa wa Morogoro mtibwa Sugar mechi iliyochezwa leo.
Baada ya matokeo hayo Simba wanaendelea kusalia kileleni wakiwa na alama 45 akiwa mebel kwa alama mbili dhidi ya mahasimu wao Yanga wenye alama 43 baada ya mechi yao ya jana kushinda dhidi ya Majimaji Songea.

Baada ya mchezo huu Simba wanakutana na Azam Januari 28 kwenye Uwanja wa Taifa.


Henry Joseph akipambana na mchezaji wa Simba Mwinyi Kazimoto katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.

Kipa wa Mtibwa akiondosha mpira langoni mwake katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.

Wachezaji wakiwa wanasubiri kupigwa kwa mpira langoni mwa Simba.

Mshambuliaji wa Simba Shiza Kichuya akiwa amemfanyia madhambi Rashidi Mandawa katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.


Mshambuliaji wa Simba Juma Luizio akiwa anapambana na beki wa Mtibwa Henry Joseph katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.

Kiungo wa Mtibwa Ally Shomari akipambana na beki wa Simba Hamad Juma katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.

Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akiutuliza mpira pembeni mwa mabeki wa Mtibwa katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.

Kipa wa Simba Daniel Aggey akidaka mpira uliopigwa na Rashid Mandawa wa Mtibwa Sugar katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.Picha zote na Zainab Nyamka.