Tuesday, January 17, 2017

VPL: MABINGWA YANGA WAITUNGUA BAO 1-0 TIMU YA MAJIMAJI FC, WAJISOGEZA KARIBU NA SIMBA KILELENI!

VPL, Ligi Kuu Vodacom, Leo imeendelea huko Uwanja wa Majima Mjini Songea wakati Majimaji FC ilipofungwa 1-0 na Mabingwa Watetezi Yanga.
Bao la ushindi la Yanga lilipachikwa Dakika ya 14 na Deus Kaseke.
Matokeo haya yamewaweka Yanga kuwa Pointi 1 nyuma ya Vinara Simba ambao kesho wapo huko Jamhuri Jijini Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar. Mechi nyingine ambayo pia itachezwa kesho ni huko Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kati ya Azam FC na Mbeya City.


MSIMAMO:
1. Simba SC Mechi 18 Pointi 44
2. Young Africans 19 43
3. Kagera Sugar 19 31
4. Azam FC 18 30

5. Mtibwa Sugar 18 30
6. Stand United 19 25
7. Mbeya City 18 24
8. Ruvu Shooting 19 24
9. Tanzania Prisons 18 22
10. Mwadui FC 19 22
11. African Lyon 18 20
12. Mbao FC 18 19
13. Ndanda FC 19 19
14. Majimaji 19 17
15. Toto Africans 18 16
16. JKT Ruvu 19 15