Saturday, January 28, 2017

WENGER AFUNGIWA MECHI 4, NA FAINI JUU, LEO KUIKOSA MECHI NA SOUTHAMPTON!

MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amefungiwa Mechi 4 na kutwangwa Faini ya Pauni 25,000 na FA, Chama cha Soka England, kwa Kosa la Utovu wa Nidhamu alipopatikana na hatia ya kumkashifu Refa na pia kumsukuma Refa Msaidizi.

Wenger, mwenye Miaka 67, alimsukuma Refa Msaidizi Anthony Taylor baada ya Refa wa Mechi yao na Burnley Jon Moss kumuamuru kutoka Uwanjani kwa kutoa Lugha chafu.

Kifungo cha Wenger kinaanza kwa Mechi ya Leo Ugenini na Southampton huko Saint Mary ikiwa ni Mechi ya Raundi ya 4 ya FA CUP.
Mechi nyingine atakazozikosa ni zile za EPL, Ligi Kuu England dhidi ya Watford, Chelsea na Hull City.

Ikiwa Mechi ya Leo itaisha Sare basi Arsenal watarudiana na Southampton huko Emirates na hiyo itahesabika kwenye Kifungo na hivyo Kifungo chake kitaisha Mechi na Chelsea.

Kifungo cha Wenger ni cha kumkataza kukaa Benchi la Ufundi tu na hivyo ni ruhusa kuwepo kwake Uwanjani.
Klopp afanya mabadiliko 9 kwenye kikosi chake leo wakikaribia muda mchache ujao kuumana na Wolverhampton Wanderers