Saturday, February 4, 2017

AFCON 2017: CAMEROON YAITEKETEZA GHANA, FAINALI SASA NI EGYPT vs CAMEROON JUMAPILI.

African Cup of Nations 2017 (AFCON 2017) Final (Egypt vs Cameroon) Match ScheduleCAMEROON wameingia Fainali ya AFCON 2017, Kombe la Mataifa ya Afrika, baada kuifunga Ghana 2-0 Leo huko Nchini Gabon.
Mechi hii, Ghana walionekana wako juu kidogo lakini kukosa kwao umakini kwa nafasi chache walizopata ndio hasa kumesababisha wapigwe.

egypt cameroonFrikiki ya Dakika ya 71 ilizaa Bao kwa Cameroon pale Difensi ya Ghana ilipojichanganya na kumruhusu Ngadeu kufunga.
Ndani ya Dakika za Nyongeza, kaunta ataki ya Cameroon ilizaa Bao lao la pili kwa Bassogog kuchanja mbuga na Mpira na kumchambua Kipa Brimah na kuipa Cameroon ushindi wa 2-0.
Sasa Cameroon watacheza Fainali na Egypt hapo Jumapili kupata Bingwa wa Afrika wakati Ghana wakicheza Jumamosi na Burkina Faso kusaka Mshindi wa Tatu.
VIKOSI:
CAMEROON:
Ondoa, Oyongo, Fai, Ngadeu, Teikeu, Siani, Djoum, Zoua, Moukandjo, Bassogog, Tambe

GHANA:
Brimah; Acheampong, Afful, Amartey, Boye; Wakaso, Acquah, Partey, Atsu, Andre Ayew, Jordan Ayew
REFA: B Gassama (Gambia)
Video: Cameroon 2 – 0 Ghana (February-2-2017) African Cup of Nations 2017 (AFCON 2017) SemifinalMshindi wa 3
Jumamosi Februari 4

22:00 Burkina Faso v Ghana

Fainali
Jumapili Februari 5

22:00 Egypt v Cameroon

NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA:

-Egypt-Mara 7
-Cameroon, Ghana-Mara 4
-Nigeria-Mara 3
-Congo DR-Mara 2
-Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan, Tunisia-Mara 1