Sunday, February 5, 2017

AFCON 2017: EGYPT 1 vs 2 CAMEROON, NICOLAS NA VINCENT WAIONGOZA CAMEROON KULIPA KISASI NA KUTWAA KOMBE!

CAMEROON usiku huu huko Libreville, Gabon, walitoka nyuma kwa Bao 1 na kuibwaga Egypt 2-1 na kutwaa Ubingwa wa Mataifa ya Afrika katika Mashindano ya 31 ya AFCON 2017, Kombe la Mataifa ya Afrika.
Hii ni mara ya kwanza kwa Cameroun kuifunga Egypt katika Fainali 3 walizokutana nayo huko nyuma na hii ni mara yao ya kwanza kutwaa Ubingwa wa Afrika tangu Mwaka 2002 ilipokuwa mara yao ya 4 kuwa Bingwa.
Egypt ndio waliotangulia kufunga katika Dakika ya 22 Mfungaji akiwa Kiungo wa Arsenal Mohamed Elneny na Bao hilo kudumu hadi Haftaimu.

Kipindi cha Pili, Wachezaji Wawili wa Cameroon walioanzia Benchi ndio waligeuza Mechi pale Nicolas N’Koulou aliposawazisha Dakika ya 59 na Vincent Aboubakar kuwapa ushindi Dakika ya 88.
Bao hizo ziliamsha nderemo na vifijo miongoni mwa Mashabiki 38,000 wengi wao wakiwa ni wa Cameroon.


VIKOSI:
EGYPT:
Essam El Hadary, Ahmed Fathi, Ahmed Hegazy, Ali Gabr, Ahmed Elmohamady, Mohamed Elneny, Tarek Hamed, Amr Warda, Abdallah Said, Mahmoud Hassan (Ramadan Sobhi 66’), Mohamed Salah

CAMEROON:
Fabrice Ondoua, Michael Ngadeu-Ngadjui, Collins Fai, Adolphe Teikeu (Nicolas N’Koulou 32’), Ambroise Oyongo, S├ębastien Siani, Arnaud Sutchuin Djoum, Benjamin Moukandjo, Robert Ndip Tambe (Vincent Aboubakar 46’), Christian Bassogog, Jacques Zoua (Georges Mandjeck 90+4’)
http://a1.espncdn.com/combiner/i?img=%2Fphoto%2F2017%2F0205%2Fr178232_1296x518_5%2D2.jpg&w=1006&h=402&scale=crop&cquality=80&location=originBao la Egypt lilifungwa na Mohamed Elneny dakika ya (22')
Huku Nicolas N'Koulou akiisawazishia bao dakika ya (59') kipindi cha pili na dakika za lala salama Vincent Aboubakar aliipa bao dakika ya (88') na mtanange kumalizika kwa 2-1.Cameroon's Belgian coach Hugo Broos Shabiki wa CameroonFIFA president Gianni Infantino(katikati)
N'Koulou's akitupia kwa kichwa
Cameroon wakiwa kwenye shangwe

Egypt wakipagawa baada ya Camerron kusawazisha bao
Aboubakar
Shangwe kwa Cameroon
Mchezaji wa Cameroon  Collins Fai akipeta Elneny akipagawa baada ya kuona bao linachomolewa na kuongezwa tena
Wachezaji wa  Cameroon wakipongezana