Wednesday, February 1, 2017

AFCON 2017 - NUSU FAINALI: LEO HUKO GABON NI BURKINA FASO vs EGYPT

Leo huko Stade d'Angondje Mjini Angondjé Nchini Gabon Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya AFCON 2017, Mashindano ya 31 ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, itachezwa kati ya Burkina Faso ambao hawajawahi kutwaa Kombe hili na Egypt ambao ndio Vigogo wa Ubingwa huu kwa kuutwaa mara 7.
Egypt, chini ya KochaHector Cuper, wataingia kwenye Mechi hii bila Kiungo wa Arsenal Mohamed Elneny ambae ni Majeruhi huku StraikaMarwan Mohsen akiwa na hatihati kutokana na maumivu ya Goti.
Lakini Vigogo hawa wa Afrika bado ni ngangari na walianza Mashindano haya kwa Sare ya 0-0 na Mali na kisha kushinda 1-0 katika Mechi zao zilizofuata dhidi ya Uganda, Ghana na Morocco.
Difensi ya Egypt, ipo chini ya Kipa mkongwe Essam El Hadary alietimiza Miaka 44 Januari na kuweka Rekodi ya kiwa Mchezaji mwenye Umri mkubwa kuwahi kuichezea AFCON.
El Hadary alikuwemo kwenye Kikosi cha Egypt kilichoenda Nchini Burkina Faso Miaka 19 iliyopita na kwenye Nusu Fainali za AFCON kuwatoa Wenyeji hao na kutinga Fainali walikotwaa Ubingwa.
Burkina Faso wametinga Nusu Fainali licha kupata msukosuko wa kuwapoteza Wachezaji wao Wawili wakubwa kwenye Raundi ya mwanzo.
Jonathan Pitroipa, ambae ndie aliteuliwa Mchezaji Bora wa Fainali za AFCON 2013, na Jonathan Zongo wote waliumia na kuondoka nje ya Mashindano.

Nguzo kubwa ya Burkina Faso ni Kipa wao Herve Koffi mwente Miaka 20 amvae amefungwa Bao 2 tu kwenye AFCON 2017.
Mbele ya Kipa huyo husimama Bakary Kone, Kepteni Charles Kabore na Prejuce Nakoulma huku Mtu wao hatari ni Steaika wao Aristide Bance.
Kesho Alhamisi Usiku ipo Nusu Fainali nyingine irakayochezwa huko Mjini Franceville kati ya Cameroon na Ghana ambazo zote zimetwaa Ubingwa huu mara 4 kila mmoja.