Saturday, February 25, 2017

CLAUDIO RANIERI AFUKUZWA LEICESTER CITY, NI BAADA YA MIEZI 9 TU BAADA KUWAPA UBINGWA ENGLAND

MABINGWAwa England LeicesterCity wamemfukuza kazi Meneja wao ikiwa ni Miezi 9 tu baada ya kuwapa, bila kutegemewa, Ubingwa wao wa kwanza wa England katika Historia yao.
Habari hizi zimetolewa na Bodi ya Leicester City na zimekuja Siku 1 tu baada ya Klabu hiyo kufungwa 2-1 huko Spain na Sevilla katika Mechi yao ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Ranieri, mwenye Miaka 65, aliiongoza Leicester, kwa mshangao wa wengi, kutwaa Ubingwa wa England Msimu uliopita wakiwa mbele kwa Pointi 10 lakini Msimu huu mambo yako mrama na wako hatarini kuporomoka Daraja.
Likitokea hilo basi wao ndio watakuwa Mabingwa Watetezi wa kwanza wa England kushuka Daraja tangu 1938.
Leicester wamepoteza Mechi zao 5 za Ligi zilizopita na ndio Klabu pekee katika Madaraja yote Manne ya England ambayo haijafunga hata Bao 1 la Ligi Mwaka huu 2017.
Mechi ijayo kwa Leicester ni kwao King Power Stadium Jumatatu ijayo dhidi ya Liverpool.