Wednesday, February 1, 2017

COPA DEL REY: LEO NUSU FAINALI ATLETICO MADRID vs BARCELONA HUKO VICENTE CALDERON

LEO UWANJA wa Vicente Caldero Jijini Madrid Nchini Spain ndio dimba la Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la Mfalme wa Spain, Copa del Rey, kati ya Atlético Madrid na Barcelona.
Mechi ya Pili kati yao itachezwa huko Nou Camp Wiki ijayo.
Hali za Timu
Kwenye Mechi hii Barca hawatamtumia Kipa Marc-André ter Stegen ambae hucheza La Liga tu na badala yake langoni atakuwepo Jasper Cillessen.
Pia watawakosa Majeruhi Andrés Iniesta, Sergio Busquets na Lucas Digne.

Kwa upande wa Wenyeji Atlético Madrid walio chini ya Kocha Diego Simeone wao watamkosa José Giménez kwenye Difensi lakini nafasi yake itachukuliwa na Stefan Savic ambae atadabo na Diego Godín.
Wengine wanaotarajiwa kuanza pambano hili ni Kiungo Juanfran na pia wapo Ferreira Carrasco na Antoine Griezmann.
Nusu Fainali nyingine ya Copa del Rey itachezwa Kesho huko Estadio Municipal de Balaidos kati ya Celta Vigo na Deportivo Alaves.