Saturday, February 25, 2017

DABI DAR: SIMBA 2 vs 1 YANGA.

Image may contain: 2 people, stadium and outdoorDabi ya Kariakoo uliochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Leo ulishuhudia Mtu Simba ikitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuichapa Yanga 2-1.
Yanga walifunga Bao lao Dakika ya 5 kwa Penati ya Simon Msuva iliyotolewa baa Fowadi wao Obrey Chirwa kuangushwa na Beki Novatus Lufunga.

Image may contain: 8 people, people standing, stadium, grass and outdoorDakika ya 55 Simba walibaki Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Janvier Besala Bokungu kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya kulambwa Kadi za Njano 2.
Simba wakasawazisha Bao Dakika ya 66 kupitia Laudit Mavugo aleingizwa Kipindi cha Pili na kufunga Bao la Pili na la ushindi Dakika ya 81 Mfungaji akiwa Shiza Kichuya.
VPL, inayoshirikisha Timu 16, sasa inaongozwa na Simba wenye Pointi 54 kwa Mechi 23 na Yanga ni wa Pili wakiwa na Pointi 49 kwa Mechi 22 huku Azam FC ni wa 3 wakiwa na Pointi 41 kwa Mechi 23.
VIKOSI:
SIMBA:
Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga [Shiza Kichuya, 51’], Abdi Banda, James Kotei, Ibrahim Hajib, Muzamil Yassin, Juma Luizio [Said Ndemla, 27’], Laudit Mavugo, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim [Jonas Mkude, 57’].

YANGA:
Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Andrew Vincent, Kevin Yondan, Justine Zulu [Juma Mahadhi, 78’], Simoni Msuva, Thabani Kamusoko [Said Juma ‘Makapu’, 45’], Amisi Tambwe [Deus Kaseke, 70’], Obrey Chirwa, Haruna Niyonzima.

REFA:
Mathew Akrama [Mwanza]
WASAIDIZI: Mohammed Mkono [Tanga] na Hassan Zani [Arusha]