Tuesday, February 7, 2017

EFL CUP – FAINALI MANCHESTER UNITED vs SOUTHAMPTON REFA NI ANDRE MARRINER

REFA Andre Marriner amethibitishwa kuwa ndie Refa wa Fainali ya Kombe la Ligi huko England, EFL CUP, kati ya Manchester United na Southampton ambayo itachezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Jumapili Februari 26.
Refa Marriner, mwenye Miaka 46, atasaidiwa na Richard West na Stuart Burt wakati Kevin Friend akiwa Refa wa Akiba.

Msimu huu, katika Mechi 24 alizochezesha, Refa Marriner ametoa Kadi za Njano 92 na Kadi Nyekundu 5.
Mapema mwanzoni mwa Msimu huu, Marriner aliiminya Man United Penati ya wazi walipotoka Sare 1-1 na Arsenal Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Baada ya Mechi hiyo, Meneja wa Man United Jose Mourinho, alikataa kumponda Refa Andre Marriner akidai ni ‘Mtu Mkweli na Refa mzuri.’
Alisema: “Sitaki kuzungumzia hilo. Nina hisia nzuri kuhusu Andre Marriner. Yeye ni aina ya Refa akifanya makosa kuhusu Timu yangu najua hana nia.”
EFL CUP
Fainali
Jumapili Februari 26

19:30 Manchester United v Southampton