Thursday, February 2, 2017

EPL: MAN CITY YAISHUSHIA KIPIGO KIZITO WEST HAM, MAN UNITED YABANWA MBAVU, STOKE CITY NA EVERTON NAO WALALA KWA SARE!

Ligi Kuu England imeendelea Jana kwa Mechi 3 na Manchester City kuibuka washindi wakubwa kwa kuicharaza West Ham 4-0 wakati Manchester United ikitoka 0-0 na Hull City na Stoke City na Everton kutoka 1-1.
Huko London Stadium Jijini London, Wenyeji West Ham walibandikwa Bao 4-0 na Man City kwa Bao za Kevin De Bruyne, David Silva, Gabriel Jesus na Yaya Toure.
Matokeo hayo yamewabakisha City Nafasi ya 5.
Huko Old Trafford, Kipa wa Hull City Eldin Jakupovic aliikosesha ushindi Man United kwa kuokoa Bao za wazi kadhaa na hasa michomo ya Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba.
Matokeo hayo yamewabakisha Man United Nafasi ya 5 ingawa hawajafungwa katika Mechi zao 14 zilizopita za Ligi lakini Sare hii ya 3 mfululizo ndio inawatafuna na kuwabakisha Nafasi hiyo ya 6 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya 5 City na Liverpool zinazofungana kwa Pointi.

Huko Britannia Stadium, Wenyeji Stoke City na Everton zilitoka Sare 1-1 na Wafungaji walikuwa Peter Crouch kwa Stoke na Ryan Shawcross aliejifunga mwenyewe kuisawazishia Everton.

Kwa Crouch, hilo lilikuwa Bao lake la 100 la Ligi. 


EPL – Ligi Kuu England

RATIBA
Jumamosi Februari 4

1530 Chelsea v Arsenal
1800 Crystal Palace v Sunderland
1800 Everton v Bournemouth
1800 Hull City v Liverpool
1800 Southampton v West Ham United
1800 Watford v Burnley
1800 West Bromwich Albion v Stoke City
2030 Tottenham Hotspur v Middlesbrough

Jumapili Februari 5

1630 Manchester City v Swansea City

1900 Leicester City v Manchester United