Saturday, February 11, 2017

FULL TIME: ARSENAL 2 vs 0 HULL CITY, WENGER ALISHANGAA BAO LA MKONO!

Alexis Sanchez Leo amefunga Bao 2, moja kwa Mkono na jingine kwa Penati, na kuipa Arsenal ushindi wa 2-0 walipocheza kwao Emirates na Hull City katika Mechi ya kwanza kabisa hii Leo ya EPL Ligi Kuu England.
Arsenal walifunga Bao la Kwanza Dakika ya 34 baada ya Mpira kumgonga Mkononi na kutinga kufuatia kizaazaa cha Krosi Kieron Gibbs.
Bao la Pili la Arsenal lilifungwa tena na Sanchez katika Dakika za Majeruhi, Dakika ya 92, kwa Penati iliyotolewa baada ya Sam Clucas kuushika Mpira wa Kichwa wa Lucas Perez kwenye Mstari wa Goli.

Refa Mark Clattenburg aliwapa Penati Arsenal na kumpa Kadi Nyekundu Sam Clucas na Sanchez kufunga Penati hiyo. Ushindi huu umewaweka Arsenal Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 50 sawa na Tottenham ambao wako Nafasi ya Pili lakini wanacheza baadae Leo huko Anfield na Liverpool.

VIKOSI:
ARSENAL:
Cech, Bellerin, Mustafi, Koscielny, Gibbs, Oxlade-Chamberlain, Coquelin, Walcott, Ozil, Iwobi, Sanchez.
Akiba: Gabriel, Lucas Perez, Giroud, Ospina, Monreal, Welbeck, Elneny.

Hull City: Jakupovic, Elabdellaoui, Ranocchia, Maguire, Robertson, Huddlestone, N’Diaye, Markovic, Grosicki, Clucas, Niasse.
Akiba: Meyler, Maloney, Diomande, Marshall, Elmohamady, Tymon, Evandro.
REFA: Mark Clattenburg