Sunday, February 12, 2017

FULL TIME: BURNLEY 1 v 1 CHELSEA, BLUES WADUWAA SARE, BRADY NDIYE ALIYESAWAZISHA BAO!

Chelsea Leo wameikosa nafasi ya kwenda Pointi 12 mbele baada ya kutoka Sare na Burnley huko Turf Moor.
Chelsea sasa wako Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Tottenham lakini Jumatatu Usiku Manchester City wanaweza kutwaa Nafasi ya Pili na pengo lao na Chelsea kuwa Pointi 8 ikiwa wataifunga Bournemouth Ugenini.

Hii Leo Chelsea walitangulia kufunga Dakika ya 7 kwa Bao la Pedro lakini Robbie Brady akaisawazishia Burnley Dakika ya 24 kwa Frikiki kali.

Matokeo haya yanawaweka Burnley Nafasi ya 12 na kudumisha rekodi yao ya kuwa wagumu mno wakiwa kwao Turf Moor.