Wednesday, February 1, 2017

FULL TIME EPL, ARSENAL 1 vs 2 WATFORD

Wakicheza huku Meneja wao Arsene Wenger akiwa Jukwaani kwa Watazamaji badala ya Benchi akitumia Kifungo cha Mechi 4 na hii ikiwa ni ya pili kwake, Arsenal walibwagwa na Watford ambao ndani ya Dakika 2 na Sekunde 57 walipiga Bao 2 na kuongoza 2-0.2-0IwobiBao la Kwanza la Watford lilifungwa na Younes Kaboul Dakika ya 10 na la pili kupigwa Dakika ya 13 na Troy Deeney. Arsenal walipata Bao lao Dakika ya 58 kupitia Alex Iwobi.
Leo hii EPL itaendelea kwa Mechi 3 wakati Man United wakiwa kwao Old Trafford kucheza na Hull City, Man City wakiwa Wageni wa West Ham huko London Stadium Jijini London na Stoke City kuikaribisha Everton.