Wednesday, February 1, 2017

FULL TIME EPL, LIVERPOOL 1 vs 1 CHELSEA

CHELSEA wameendelea kupeta kileleni mwa EPL, Ligi Kuu England, licha ya Jana Diego Costa kukosa Penati ambayo ingewapa ushindi na kuambua Sare ya 1-1 Ugenini huko Anfield walipocheza na Liverpool.

Chelsea walitangulia kufunga Dakika ya 24 kwa Frikiki ya David Luiz na Liverpool kusawazisha Dakika ya 57 kwa Bao la Georginio Wijnaldum.

Zikibaki Dakika 14, Refa Mark Clattenburg aliwapa Penati Chelsea baada Diego Costa kuangushwa na Joel Matip na Costa kupiga Penati hiyo iliyochezwa vizuri na Kipa Simon Mignolet.

Baada Mechi 23, Chelsea wapo kileleni wakiwa na Pointi 56 na wa Pili ni Tottenham wenye 47 pamoja na Arsenal wenye 47 baada ya Jana Tottenham kutoka 0-0 na Sunderland huko Stadium of Light wakati Arsenal, wakiwa Nyumbani Emirates Jijini London, ikitwangwa 2-1 na Watford