Saturday, February 4, 2017

FULL TIME VPL: MAJI MAJI 0 vs 3 SIMBA

Simba Leo huko Uwanja wa Majimaji Mjini Songea wameichapa Maji Maji FC 3-0 katika ya VPL, Ligi Kuu Vodacom, na kuwakaribia Vinara Yanga wakiwa Pointi 1 nyuma yao.
Hadi Mapumziko Simba walikuwa mbele 1-0 kwa Bao la Dakika ya 19 la Ibrahim Ajib na Kipindi cha Pili kufunga Bao nyingine 2 kupitia Said Ndemla Dakika ya 63 na Laudit Mavugo Dakika ya 88.
Simba sasa wana Pointi 48 kwa Mechi 21 huku Yanga wakiongoza wakiwa na Pointi 49 kwa Mechi 21 pia.
Timu ya 3 ni Kagera Sugar iliyocheza Mechi 21 na wana Pointi 37 wakifuatia Azam FC wenye Pointi 34 kwa Mechi 20.


VPL – Ligi Kuu Vodacom
RATIBA:
Jumatatu Februari 6

Toto Africans v Ruvu Shooting
Mbeya City v JKT Ruvu


Jumanne Februari 7

Azam FC v Ndanda FC

Jumatano Februari 8

Tanzania Prisons v JKT Ruvu