Friday, February 10, 2017

LISTI FIFA/COCA COLA UBORA DUNIANI: ARGENTINA BADO 1, BRAZIL 2, EGYPT JUU AFRIKA, TANZANIA YAPOROMOKA MPAKA 158

FIFA Leo imetoa Listi mpya ya ubora Duniani kwa nchi Wanachama wake, ambayo huitwa Listi ya FIFA/Coca Cola Ubora Duniani, na Vinara wake bado ni Argentina wakifuatia Brazil na kwa Afrika Egypt ndio wapo juu kabisa huku Tanzania ikishuka Nafasi 2 na kukamata Namba 158.
5 Bora kwenye listi hiyo zimebaki zile zile bila mabadiliko na nazo ni Argentina (1), Brazil (2), Germany (3), Chile (4) na Belgium (5).

Kwa Afrika, Nchi ambayo iko juu kabisa ni Egypt, waliotolewa Fainali ya AFCON 2017, ambao sasa wapo Nafasi ya 23 baada kupanda Nafasi 12 wakifuata Senegal walio Nafasi ya 31 na Mabingwa Wapya wa Afrika ambao ndio waliwafunga Egypt, Cameroun, wapo Nafasi ya 33 baada kupaa Nafasi 29.

Listi nyingine ya FIFA/Coca Cola Ubora Duniani itatolewa itatolewa Tarehe 9 Machi 2017.


FIFA LIST YA UBORA DUNIANI – 20 BORA:
NAFASI
NCHI
NAFASI ILIZOPANDA AU KUSHUKA
1
Argentina
0
2
Brazil
0
3
Germany
0
4
Chile
0
5
Belgium
0
6
France
1
7
Colombia
-1
8
Portugal
0
9
Uruguay
0
10
Spain
0
11
Switzerland
0
12
Wales
0
13
England
0
14
Poland
1
15
Italy
1
16
Croatia
-2
17
Mexico
1
18
Peru
1
19
Costa Rica
-2
20
Iceland
1