Sunday, February 26, 2017

FULL TIME... EFL CUP: MANCHESTER UNITED 3 vs 2 SOUTHAMPTON, IBRAHIMOVIC AIPA KOMBE UNITED!


ZLATAN IBRAHIMOVIC amepiga Bao 2 wakati Manchester United wakiifunga Southampton, maarufu kama ‘Watakatifu’, 3-2 katika Fainali ya Kombe la Ligi huko England, EFL CUP, iliyochezwa Uwanjani Wembley Jijini London.

Mbali ya Ibrahimovic kudumisha Rekodi yake ya kufunga Bao muhimu na kutwaa Makombe Nchi mbalimbali huko Ulaya, Meneja wa Man United, Jose Mourinho, ameweka Rekodi ya kutwaa Kombe hili mara 4 na kuungana na Brian Clough na Sir Alex Ferguson ambao pia wamelitaa mara Nne.
Mourinho alibeba Kombe hili mara 3 akiwa na Chelsea.

Man United walitangulia 2-0 kwa Bao za Zlatan Ibrahimovic, kwa Frikiki, na Jesse Lingard, lakini Mchezaji wao mpya Southampton alietua kwao Januari kutoka Italy Manolo Gabbiadini aliwapa matumaini kwa kuwapa Bao kabla Haftaimu na Gemu kuwa 2-1.

Kipindi cha Pili Dakika ya 48 Manolo Gabbiadini tena akafunga Bao na Gemu kuwa 2-2.
Zikibaki Dakika 3, huku Mourinho akiwa tayari kumuingiza Kepteni wao Wayne Rooney, Man United walianza kaunta ataki na kisha Krosi tamu ya Ander Herrera ilitua Kichwani mwa Zlatan Ibrahimovic aliefunga Bao la 3.
Hapo hapo Mourinho akamrudisha Rooney Benchi na kumuingiza Maroune Fellaini badala ya Anthony Martial ili kuimarisha ulinzi.

LAKINI KIKUBWA NI KUWA JOSE MOURINHO AMEKUWA MENEJA WA KWANZA KATIKA HISTORIA YA MAN UNITED KUTWAA KOMBE KATIKA MSIMU WAKE WA KWANZA. 3-22-2