Saturday, February 11, 2017

FULL TIME: MANCHESTER UNITED 2 vs 0 WATFORD, MARTIAL NA MATA WAIPA MATUMAINI UNITED OLD TRAFFORD! UNITED WAWEKA REKODI YA POINTI NYINGI ZAIDI

Martial kaipa bao la pili Man United na kufanya 2-0 dhidi ya Timu ya Watford.
 MAN UNITED wameifunga Watford 2-0 kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, na kung;oka Nafasi ya 6 waliyoshikilia muda mrefu na sasa wapo Nafasi ya 5 na watabakia hapo labda baadae Leo Liverpool iifunge Tottenham.

Bao za Man United hii Leo zilifungwa katika kila Kipindi na Juan Mata, Dakika ya 32, na Anthony Martial Dakika ya 60 huku wakikosa lukuki ya Mabao.
Ushindi huu umewaweka Man United Nafasi ya 5 wakiwa na Pointi 48 na Pointi hizi 3 za Leo zimewafanya wafikishe Pointi 2,000 kwenye Ligi huko England na kuweka Rekodi mpya.
Pia sasa Man United wako kwenye mbio za Mechi 16 bila kufungwa kwenye EPL.

Mata akishangilia bao lake la kwanza kwa Man United jioni hii