Wednesday, February 15, 2017

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: PSG 4 vs 0 BARCELONA, USIKU MBAYA WA BARCA!

Jana huko Parc des Princes Jijini Paris Nchini France Mabingwa wa huko Paris St Germain waliifumua Barcelona 4-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI.
Kwenye Mechi nyingine ya Raundi hiyo Benfica iliichapa Borussian Dortmund 1-0.
Katika Mechi ya PSG na Barca, Bao za PSG zilipigwa na Angel Di Maria, Dakika za 18 na 55, Julian Draxler, 40', na Edinson Cavani, 71'.
PSG walitawala Mechi hii na Barca kupooza mno huku Mastaa wao Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar 'wakijificha'.
Kipigo hiki kinaiweka Barca pagumu kufuzu kwenda Robo Fainali na wakishindwa hilo hii itakuwa mara ya kwanza kwao kutotinga Robo Fainali katika Miaka 10.