Thursday, February 23, 2017

UEFA EUROPA LEAGUE: SAINT ETIENNE 0 vs 1 MANCHESTER UNITED

Henrikh Mkhitaryan Manchester United wakiwa huko Stade Geoffroy Guichard Uwanja wa Jijini Saint Etienne Nchini France wameifunga Saint-Etienne 1-0 katika Mechi ya Pili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI na kusonga Raundi ijayo kwa Jumla ya Bao 4-0 kwa Mechi 2.
Alhamisi iliyopita huko Old Trafford Man United waliichabanga Saint-Etienne 3-0 kwa Hetitriki ya Zlatan Ibrahimovic.

Bao la ushindi la Man United lilifunbwa Dakika ya 16 kupitia Mkhitaryan alieunganisha Pasi ya Juan Mata.
Lakini Dakika ya 25 Mkhitaryan akaumia na kubadilishwa na Marcus Rashford.
Kipindi cha Pili Dakika ya 63, Sentahafu wa Man United Eric Bailly alipewa kilaini Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu na Refa Mjerumani Deniz Aytekin.

Ijumaa Man United watajua nani mpinzani wao kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 baada ya kufanyika Droo ya kupanga Mechi hizo.

VIKOSI:
SAINT ETIENNE:
Ruffier; Malcuit, Perrin, Théophile-Catherine, Pogba; Pajot, Veretout [Lemoine, 68']; Hamouma, Saivet [Intima, 53’], Monnet-Pacquet; Besic [Roux, 58’]
Akiba: Moulin, Lacroix, Roux, Seinaes, Intima, Pierre-Gabriel

MAN UNITED:
Romero; Young, Bailly, Smalling, Blind; Fellaini, Carrick [Schweinsteiger, 61’], Pogba; Mata [Rojo, 63’], Ibrahimovic, Mhitaryan [Rashford, 25']
Akiba: De Gea, Rojo, Martial, Lingard, Rashford, Valencia, Schweinsteiger
REFA: Deniz Aytekin (Germany)