Wednesday, February 1, 2017

UHAMISHO JANUARI 2017: DILI KUBWA LIGI KUU ENGLAND

JANA Usiku wa manane Dirisha la Uhamisho lilifungwa na zifuatazo ni taarifa za dili kubwa 10 zilizofanyika kwa Klabu za EPL, Ligi Kuu England.
Gabriel Jesus
-Palmeiras (Brazil) kwenda Manchester City, £27 Milioni
Jesus, Miaka 19, alikubali kujiunga na City tangu Mwaka Jana na dili kukamilika rasmi mapema Januari.
Kijana huyo nyota wa Timu ya Taifa ya Brazil ameshaichezea City Mechi 2 hadi sasa.
Morgan Schneiderlin
-Manchester United kwenda Everton, £20 Milioni
Baada kukosa namba huko Man United chini ya Meneja Jose Mourinho, Mchezaji huyu wa Kimataifa wa France mwenye Miaka 27 ameamua kujiunga na Everton na kuungana tena na Meneja Ronald Koeman ambae walikuwa pamoja huko Southampton.
Wilfred Ndidi
-Genk (Belgium) kwenda Leicester City, £15 Milioni
Mabingwa Leicester wamemsaini Mchezaji huyu wa Kimataifa wa Nigeria mwenye Miaka 20 wakitumaini ataziba pengo lililoachwa na N'Golo Kante aliehamia Chelsea mwanzoni mwa Msimu.

https://pbs.twimg.com/media/C3iZET3XAAARSYQ.jpgManolo Gabbiadini
-Napoli (Italy) kwenda Southampton, £14 Milioni
Mchezaji huyu mwenye Miaka 25 na alieichezea Italy mara 6 aliwahi pia kuichezea Sampdoria huko Iraly.
Patrick van Aanholt
-Sunderland kwenda Crystal Palace, £14 Milioni
Huyu ni Beki wa zamani wa Chelsea mwenye Miaka 26 ambae pia huichezea Netherlands.
Robbie Brady
-Norwich City kwenda Burnley, £13 Milioni
Burnley wamevunja Rekodi yao ya ununuzi kwa kumsaini Brady mwenye Miaka 25 ambae ni Mchezaji wa Kimataifa wa Republic of Ireland alieanzia Soka lake huko Man United.
Saido Berahino
-West Bromwich Albion kwenda Stoke City, £12 Milioni
Baada mvutano wa Miezi 18 akishinikiza kuhama WBA, hatimae Berahino, mwenye Miaka 23 na ambae mara ya mwisho alicheza Septemba, amefanikiwa kuondoka.
Jeff Schlupp
-Leicester City kwenda Crystal Palace, £12 Milioni
Huyu ni Winga kutoka Ghana ambae Msimu uliopita aliichezea Leicester mara 24 wakitwaa Ubingwa wa EPL.
Ademola Lookman
-Charlton Athletic kwenda Everton, £11 Milioni
Lookman, mwenye 19 na ambae pia huichezea England U-20, ameweka Rekodi ya kuwa Mchezaji mwenye thanani kubwa kwa Daraja la 3 kwa kuihama Charlton inayocheza Ligi 1 kwenda EPL.
Robert Snodgrass
-Hull City kwenda West Ham United, £10.2 Milioni
Huyu ni Mchezaji wa Kimataifa wa Scotland ambae ndie alikuwa Mfungaji Bora wa Hull.