Saturday, February 4, 2017

VPL: MBAO FC YAIPIGA MTIBWA BAO 5 - 0, MWADUI YAIFUNGA 3-1 RUVU SHOOTING

IJUMAA, MABINGWA NA VINARA YANGA NA STAND UNITED.
VPL, Ligi Kuu Vodacom, imeendelea Leo kwa Mechi mbili huko Mwanza na Mwadui ambako Wenyeji wake wote, Mbao FC na Mwadui FC, kuibuka kidedea kwa ushindi mnono.
Huko CCM Kirumba, Mwanza, Mbao FC imeinyuka Mtibwa Sugar 5-0 wakati kule Mwadui Complex, Mwadui FC imeifunga Ruvu Shooting 3-1.
Bao za Mbao FC dhidi ya Mtibwa Sugar hii Leo zilipigwa na Steven Mganga, Pius Busuta, Habib Haji na 2 za Yusuph Ndikumana.
Kesho Ijumaa ipo Mechi 1 tu huko Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wakati Mabingwa Watetezi wa VPL ambao pia ndio Vinara wa Ligi hiyo, Yanga, watakapocheza Stand United ambayo katika Mechi ya Kwanza ya Ligi hii huko Shinyanga iliifunga Yanga 1-0.

VPL – Ligi Kuu Vodacom
Ratiba/Matokeo:
Alhamisi Februari 2

Mbao FC 5 Mtibwa Sugar 0
Mwadui FC 3 Ruvu Shooting 1
Ijumaa Februari 3
Yanga v Stand United


Jumamosi Februari 4
Mbeya City v JKT Ruvu
Maji Maji FC v Simba

Jumatatu Februari 5

Toto Africans v Ruvu Shooting

Jumanne Februari 7

Azam FC v Ndanda FC

Jumatano Februari 8

Tanzania Prisons v JKT Ruvu